Home » Afrika » Serikali ya Kenya inasema kuwa operesheni maalumu ya utafutaji na uokoaji

Serikali ya Kenya inasema kuwa operesheni maalumu ya utafutaji na uokoaji

18 January 2016 | Afrika

Serikali ya Kenya inasema kuwa operesheni maalumu ya utafutaji na uokoaji inaendelea nchini Somalia siku chache tu baada wanamgambo wa Al-Shabab kutekeleza shambulizi la kushtukiza kwenye kambi moja ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika na kudai kuwaua zaidi ya wanajeshi 100.

Kambi hiyo iliyoko kusino magharibi mwa nchi ya Somalia ilivamiwa na wanamgambo hao alfajiri ya siku ya Ijumaa, ikiwa ni shambulio jingine baya zaidi kutekelezwa na wanamgambo hao wakilenga kambi ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika.

Waziri wa ulinzi wa Kenya, Rachel Omamo amesema kuwa operesheni hiyo itakapokamilika raia watajulishwa ni wanajeshi wangapi wamepoteza maisha na waliofanikiwa kuokolewa toka kwenye mikono ya wanamgambo hao.

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi ya Serikali ya Kenya wala ile ya tume ya walinda amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISON iliyotolewa kueleza idadi kamili ya wanajeshi waliouawa na wanamgambo hao.

Ad