Mawakili wa Victoire Ingabire kupata ugumu wakati wanapotaka kuonana na mteja wao
Mawakili wa kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire anayetumikia kifungo cha miaka 15 jela, wamelalamika kupata ugumu wakati wanapotaka kuonana na mteja wao wakati huu wakiandaa kesi ya kupitiwa upya kwa hukumu yake katika mahakama ya Afrika.
Wakili wa Ingabire, Gatera Gashabana, amesema February 5 mwaka huu alienda kuonana na mteja wake kwa maandalizi ya kuanza kusikilizwa kwa kesi yake katika mahakama ya haki za binadamu mjini Arusha Tanzania, lakini hakuweza kukutana nae baada ya kuzuiwa na maofisa wa gereza.
Katika barua yake kwa rais Paul kagame, wakili wa Ingabire, alimueleza rais Kagame namna ambavyo mteja wake ananyimwa haki na kumtaka aingilie kati suala hilo ambalo anasema linamnyima haki kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha FDU.