Mapigano nchini Syria yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 280,000
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry ameionya Urusi kuwa, uvumilivu wa Marekani kuhusu vita vinavyoendelea na hatima ya raia Bashar Al Assad kuendelea kuwa madarakani unafika mwisho.
Akiwa ziarani nchini Norway, Kerry amesema ni muhimu kwa Urusi kuelekwa kuwa uvumilivu wa nchi yake una mwisho, na kusisitiza kuwa rais Assad ni lazima awajibishwe kutokana na vita vinavyoendelea tangu mwaka 2011.
Aidha, amesema Marekani iko tayari kuhakikisha kuwa uwajibikaji huo unatekelezwa ikiwa ni pamoja na viongozi wa upinzani ambao wamekuwa wakisababisha mwafaka kutopatikana.
Mazungumzo ya amani ya kumaliza vita vya miaka mitano nchini humo yamekwama na haifahamiki ni lini yatarejelewa.
Serikali ya Syria inasema kwa sasa lengo lake ni kupambana na wapiganaji wa Islamic State, huku waasi wakiendelea kuishtumu jehsi la Syria na Urusi kuendelea kuwashabulia raia katika ngime yake mjini Allepo.
Mapigano nchini Syria yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 280,000 na kusababisha Mamilioni ya watu wengine kuwa wakimbizi tangu mwezi Machi mwaka 2011.