Home » Afrika » Maelfu ya waandamanaji wapinga rais Joseph Kabila kutowania tena urais mwezi Novemba

Maelfu ya waandamanaji wapinga rais Joseph Kabila kutowania tena urais mwezi Novemba

20 April 2016 | Afrika

Polisi mjini Lubumbashi Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamepambana na maelfu ya waandamanaji wa upinzani wanaomtaka rais Joseph Kabila kutowania tena urais mwezi Novemba mwaka huu.

Waandamanaji hao walionekana wenye hasira huku wakitamka, Kabila lazima aondoke, aje atue, tumechoka, walisikika wakisema mbele ya Ofisi ya chama cha UNAFEC kinachoongozwa naAntoine-Gabriel Kyungu wa Kumwanza.

Kumekuwa na madai kuwa rais Kabila ambaye muhula wake unakamilika mwezi Novemba anapanga kubadilisha Katiba ili awanie tena urais kwa muhula wa watatu.

Omar Kavota ni mwanaharakati wa maswala ya haki za binadamu na siasa kutoka Shirika la CEFADHO akiwa mjini Goma.

Ad