Kiongozi FDLR amejiondoa katika kundi
17 February 2016 | Afrika
Kiongozi wa ulinzi wa karibu na mkuu wa waasi wa kihutu wa Rwanda waliopo nchini DRCongo wa FDLR amejiondoa katika kundi hilo na kujisalimisha nchini Rwanda, duru rasmi kutoka Kigali zimethibitisha.
Kaptaine Aphrodice Nyirimpeta aliwasili Kigali Feb 12 na kupelekwa Mutobo kaskazini mwa nchi hiyo, kambi inayowapokea wapiganaji zamani na kuwapiga msasa kabla ya kujiunga na jamii.
Mkuu wa tume inayohusika na kuwarejesha katika maisha ya kiraia wapiganaji wa zamani Jean Sayinzoga amethibitisha taarifa hiyo bila hata hivyo kueleza zaidi kuhusu sababu za kujisalimisha kwa mkuu huyo wa ulinzi wa kiongozi wa ulinzi wa mwenyekiti wa kisiasa wa kundi la FDLR Gaston Rulumi Iyamuremye.