Jenerali Jean-Marie Michel Mokoko, anazuiliwa na maafisa wa usalama
Mwanasiasa wa upinzani nchini Congo Brazaville aliyewania urais mwezi Machi huu Jenerali Jean-Marie Michel Mokoko, anazuiliwa na maafisa wa usalama.Ripoti zinasema hatua ya kukamatwa kwa Jenerali huyo zimekuja baada ya mwanasiasa huyo kujadili mipango ya kumwondoa madarakani rais Sassou Nguesso kwa ushrikiano na afisa wa Inteljensia kutoka Ufaransa.
Mkanda wa Video ulionaswa mwaka 2007 umeonesha Jenerali Mokoko akizungumza na Afisa huyo wa Inteljensai kuhusu mipango ya kumpindua raia Ngueso.
Wakili wake Yvon Eric Ibouanga amesema maafisa wa polisi wanamhoji mwanasiasa huyo baada ya kuonekana kwa mkanda huo wa Video.
Aidiha wakili wake, ameongeza kuwa mahoajino hayo dhidi ya Mokoko m aliwahi kuwa Mkuu wa jeshi kati ya mwaka 1987 na 1993 ni ya awali.
Upinzani nchini humo umekuwa ukiusmhutumu uongozi wa sasa kuendelea kuiminya uhuru wao lakini pia kuiba kura wakati wa uchaguzi wa mwezi Machi.
Wakati wa uchaguzi wa mwaka huu alipata asilimia 14 ya kura zote zilizopigwa katika uchaguzi ambao rais Sassou Nguesso alitanagwzwa mshindi kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30 sasa.