Home » Afrika » Huenda kati ya wahamiaji 400 na 500 wamezama Bahari

Huenda kati ya wahamiaji 400 na 500 wamezama Bahari

20 April 2016 | Afrika

Umoja wa Mataifa unasema umetuma ujumbe wake nchini Ugiriki kuchunguza ripoti za kuzama kwa mamia ya watu waliozama katika Bahari ya Mediterranean.

Ripoti zinasema kuwa huenda kati ya wahamiaji 400 na 500 wamepoteza maisha baada ya kuzama katika Bahari hiyo.

Uchunguzi huu umetangazwa ma msemaji wa Shirika la wakibizi duniania Ariane Rummery baada ya kuzua kwa ripoti hizo kutoka kwa Mashirika yasiyokuwa ya serikali.

Inaelezwa kuwa miongoni mwa wakimbizi hao walikuw ani raia wa Somalia waliokuwa wanakwenda Ugiriki ili kupata nafasi ya kwenda kuishi barani Ulaya.

UNHCR inasema wakimbizi hao walikuwa wametokea nchini Misri na kukutana na wengine waliokuwa wametoka nchini Libya, waliohamia katika boti lililokuwa limetokea nchini Misri kabla ya kuzama baharini.

Manusura 37 wakiume, wanawake watati na mtoto wa miaka mitatu wamepatikana baada ya kuzama kwa boti hiyo.

Sio mara ya kwanza kwa mkasa kama huu kushuhudiwa katika Bahari ya Mediterranean.

 

Ad