Dkt Abdallah Possy ametaka runinga, kuajiri wakalimani wa lugha ya alama
Serikali ya Jamuhuri ya mungano wa Tanzania imevitaka vyombo vya habari nchini kutenda haki katika kutoa taarifa za habari na vipindi vingine kwa kuwazingatie makundi maalumu ya watu katika jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo Jijini Dar es Salaam,Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera, kazi, Ajira, Bunge, na Vijana,Dkt Abdallah Possy amewataka wamiliki wa vyombo vya habar nchini haswa wa runinga, kuajiri wakalimani wa lugha ya alama ambao watakuwa wakitafsiri ya habari na vipindi vingine vyenye masilahi ya taifa katika kuhakikisha kila mtanzania anapata haki yake ya msingi ya kupata habari
Aidhaa Dkt Possi amewataka wamiliki hao wa vyombo vya habari kuheshimu Sheria ya Watu Wenye Ulemavu ya Mwaka 2010, inahamasisha na inataka maeneo yote ya ajira kutoa fursa kwa watu wenye ulemavu,
Kwa upande mwingine Dkt Possi amewataka watanzania kuondokana na lugha za kibaguzi dhidi ya watu mwenye ulemavu,lugha ambazo zimechangia kundi hilo kuendelea kubaguliwa na kubaki katika hali ngumu ya Miasha