Tume ya Taifa ya Uchaguzi yakanusha taarifa ya Kuanza mchakato Kura ya Maoni
Katika taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo imesainiwa na mkurugenzi wa Uchaguzi Ndg KAilima Ramadhani, inaeleza kwamba taarifa iliyotolewa na Gazeti la Nipashe toleo Na:0578761 la tarehe 16 Februari 2016 kwamba "MCHAKATO WA KURA YA MAONI YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA UMEIVA" kwamba taarifa hizi SIO ZA KWELI NA ZINALENGA KUUPOSHOSHA UMMA WA WATANZANIA.
Aidha Tume inapenda kutoa ufafanuzi kuwa mchakato wa kuendesha kura ya maoni ya katiba Inayopendekezwa utafanyoka baada ya mambo yafuatayo kukamilika;-
1. Uchaguzi wa Zanznibar
2. Uchaguzi wa mbunge jimbo la Kijitoupele
3. Kupatikan wabunge wa viti maalumu watatu
4. Ripoti ya uchaguzi mkuu 2015
5. kukamilika kwa maandalizi ya ratiba Mbalimbali
Hivyo Tume ya taifa ya uchaguzi imewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu mpaka hapo taarifa rasmi ya Mchakato wa Katiba Inayopendekezwa zitakapo tolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Tume ya taifa ya uchaguzi Imelitaka gazeti hilo kufanya utafiti wa kina kabla ya kuandika jambo ambalo halina ukweli wowote na bila kuwasiliana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.