Watanzania watakiwa kushirikiana na China kwa ajili ya maendeleo
Waziri Mkuu mstaafu MIZENGO PINDA amewataka watanzania kutumia uhusiano uliopo kati ya TANZANIA na CHINA kujiletea maendeleo katika mambo mbalimbali hususan uchumi.
Waziri PINDA ameyasema hayo katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa KICHINA zilizofanyika jijini Dar Es Salaam na kusema ili kuwa na uchumi imara kama uchumi wa nchi ya CHINA ni lazima wananchi wawe na nidhamu ya kazi na kujituma kwa moyo mmoja.
Amewataka watanzania kutumia fursa ya ushirikiano baina ya CHINA na TANZANIA kwa kuiga ari ya ufanyaji kazi ili kuinua uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo NAPE NNAUYE amesema TANZANIA na CHINA zitaendelea kudumisha umoja na ushirikiano uliopo.
Naibu Balozi wa CHINA hapa nchini ZHANG BIAO amesema ushirikiano wa TANZANIA na CHINA umeleta mafanikio miongoni mwa nchi hizo ambapo kwa sasa CHINA ipo katika maandalizi ya kuanzisha miradi KUMI ya maendeleo hapa nchini.
Na Tatu Abdalla