Wataalamu: Biashara ya meno ya Tembo haiwezi kumalizwa hivi karibuni
Wataalamu wa mazingira wanasema kuwa biashara ya meno ya Tembo haiwezi kumalizwa hivi karibuni kwakuwa kwa sehemu kubwa wanaofanya biashara hiyo ni watu wenye ushawishi kwenye Serikali.
Akizungumza kwenye mjadala wa shirikisho la Marekani linalofanya utafiti wa kisayansi kuhusu wanyamapori, profesa wa bailojia katika chuo kikuu cha Washington, Samuel Wasser, amesema biashara hii inaongozwa na watu wachache wenye fedha na ushawishi mkubwa kwenye Serikali.
Profesa Wasser amesema kuwa utafiti uliochapishwa kwenye jarida moja la kisayansi mwaka jana, ulionesha kuwa biashara kubwa inafanyika kwenye kanda mbili za Afrika, ambazo nyingine zinalindwa kuanzia Cameroon mpaka Congo, Gabon, Afrika Mashariki na has nchi ya Tanzania.