(ICC) ishughulikie manung’uniko ya kuwawajibisha viongozi wa Afrika pekee
Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC) imetakiwa kushughulikia manung’uniko yanayohusu kuwawajibisha viongozi wa Afrika pekee ili kukifanya chombo hicho kiendelee kutoa haki na kuheshimika
Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na mahakama hiyo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa jijini Arusha nchini Tanzania, Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania Dr.Harisson Mwakyembe ameitaka mahakama hiyo kufanyia kazi manung`uniko ya bara la Afrika licha ya Tanzania kuunga mkono shughuli za mahakama hiyo lakini bado iko kwenye msimamo wa nchi hizo.
Tayari viongozi wa umoja wa Afrika katika mkutano wao wa mjini Addis Ababa hivi karibnuni walitoa pendekezo la kujitoa katika mahakama ya ICC yenye makao yake makuu The Heague nchini uholanzi
Mahakama ya Kimataifa ya makosa ya jinai ICC inaendelea na semina ya siku tano kwa wanasheria wa ndani na nje ya bara Afrika wameikuhusu namna ya kutumia mahakama hiyo kutetea haki za binadamu na utawala bora.