Balozi Dkt. A. Mahiga,akutanana na wabunge wa A.Mashariki
15 January 2016 | Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, (wanne kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Susan Kolimba, (watatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, EALA, kutoka Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji, 9wakwanza kushoto), Mh. Makongoro Nyerere (wapili kushoto), Mh. Angella Kizigha, (Wasita kutoka kushoto), naMh. Bernard Murunya). Wabunge hao walikwenda kumsalimia waziri Mahiga na kujitambuslisha ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza vikao vya bunge hilo jijini Arusha Januari 24, 2016. (K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, mapema leo Ijumaa Januari 15, 2016 amekutana na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania waliokwenda kujitambulisha na kubadilishana mawazo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Wabunge hao waliongozwa na mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, Mh. Shy-Rose Bhanji, Mh. Angella Kizigha, na Mh.Bernard Murunya.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Susan Kolimbanaye alikuwepo wakatiwa kikao hicho kifupi cha kutambuana.
Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa wabunge wa EALA kutoka Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, alisema, “Tumefika kujitambulisha kwa Mh. Waziri kama ujuavyo yeye ni mgeni kwenye wizara hiyo, tulikuwana Dkt. Mwakyembe na sasa tunaye Dk. Augustine Mhiga, kwa hivyo tuliona ni vyematukafika kujitambulisha na kutambuana.” Alisema Mh. Makongoro na kuongeza, “Lakini pia lazima utambue kuwa vikao vya EALA, vinaanza Januari 24 pale Arusha na Mh. Mahiga ndiye mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, kwa hivyo sio busara tukakutanie kule ndio maana tumeona ni vema tukaja kumsalimia hapa atutambue na kubadilishana mawazo hapa na pale.” Alimaliza Mh. Makongoro.
Bunge la Afrika Mashariki, EALA, ni chombo cha kutunga sheria cha Juamuiya ya Afrika Mashariki na linaundwa na nchiwanachama wa Jumuiya hiyo ambaonipamoja na Tanzania, inayoshikilia uenyekiti kwa sasa, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.