Tanzania
10 February 2016
Waziri wa Mali asili na Utalii wa Tanzania Profesa Jumanne Maghembe amesema Tanzania imepanga kuanzisha Kitengo maalumu cha kukabiliana na uhalifu wa Wanyamapori ikiwa kwenye juhudi ya kuzidisha mapambano yake dhidi ya ujangili.
Hatua hiyo imekuja siku chache tu tangu majangili waitungue helikopta iliyokuwa kwenye doria ya kawaida katika Hifadhi... [Read More]
09 February 2016
Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC) imetakiwa kushughulikia manung’uniko yanayohusu kuwawajibisha viongozi wa Afrika pekee ili kukifanya chombo hicho kiendelee kutoa haki na kuheshimika
Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na mahakama hiyo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa jijini Arusha nchini Tanzania, Waziri wa Katiba na... [Read More]
08 February 2016
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akihutubia wakati akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika Mchapalo wa Mwaka Mpya kwa Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Kimtaifa maarufu kama "Sherry Party" Ikulu jijini Dar... [Read More]
08 February 2016
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ataitisha kikao cha viongozi wa dini zote hivi karibuni ili wapange na kuainisha ni mambo gani ambayo wanaweza kutoa ushauri kwa Serikali na kupata njia bora ya kuwahudumia Watanzania.
Ametoa ahadi hiyo leo mchana (Jumapili, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na mamia ya waumini walioshiriki ibada ya... [Read More]
07 February 2016
HISTORIA YA CCM TANGU TANU NA ASP
Chama cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa tarehe 5 Februari, 1977 kutokana na kuvunjwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP).
Tendo hilo la kihistoria lilikuwa ni la kuendeleza utamaduni uliokuwa umeanza huko nyuma wa kuunganisha nguvu kwa lengo la kujiimarisha katika... [Read More]
07 February 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ukarabati unaondelea katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la Kibaigwa, sehemu ya barabara hiyo inakarabatiwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS
05 February 2016
Baraza ambalo litakuwa na lengo la kuishinikiza serikali ya Rais Magufuli kutimiza kile alichoahidi kwa Watanzania.
Baraza hilo ni kama ifuatavyo;
BARAZA KIVULI LA MAWAZIRI
Wizara ya Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri – Jaffar Michael
Naibu Waziri – Joseph Nkundi na Ruth Mollel
Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano... [Read More]