Uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata 43 kufanyika Novemba 26 mwaka huu
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 kuwa utafanyika Novemba 26 mwaka huu.
Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage, amesema kuwa uchaguzi huo unafanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya madiwani kufariki dunia, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa na Mahakama.
Jaji Kaijage amesema tume imetangaza kufanyika kwa uchaguzi huo mdogo, baada ya waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa kuitaarifu tume uwepo wa nafasi wazi za madiwani katika kata hizo 43 zilizoko katika halmashauri mbalimbali 36 na mikoa 19 ya Tanzania Bara.
Jaji Kaijage ameainisha kwamba kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya. 292 kinampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kuitarifu tume kuhusu kuwepo kwa uchaguzi huo mdogo wa madiwani.
Amefafanua kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Sura ya 292, Tume ya taifa ya uchaguzi ina wajibu wa kuitisha na kuendesha Uchaguzi mdogo katika Kata hizo.
“Hivyo, ninapenda kuchukua nafasi hii kutoa taarifa kuwa tume imepanga kuendesha uchaguzi mdogo katika Kata 43 tarehe 26 Novemba, 2017,” alisema Jaji Kaijage.
Amesema ratiba ya mchakato wa uchaguzi huo itaanza Oktoba 26 ambapo kutafanyika uteuzi wa wagombea udiwani na kampeni za uchaguzi huo mdogo zitaanza Oktoba 27 na kumalizika Novemba 25.
Jaji Kaijage aliema Vyama vya Siasa, Wadau wote wa Uchaguzi na Wananchi wanakaribishwa kwa ajili ya kushiriki kwenye uchaguzi huo utakaozingatia ratiba iliyoainishwa hapo juu.
Alitoa mwito kwa vyama vya Siasa na Wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2015, Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 pamoja na maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na Tume wakati wote wa Uchaguzi mdogo.
Kata ambazo zitashiriki kwenye uchaguzi huo ni kama ilivyoanishwa kwenye jedwali hapa chini:
Na |
MKOA |
HALMASHAURI |
KATA |
---|---|---|---|
1. |
ARUSHA |
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha |
Musa |
Halmashauri ya Jiji la Arusha |
Muriet |
||
Halmashauri ya Wilaya ya Meru |
Ambureni |
||
Halmashauri ya Wilaya ya Meru |
Ngabobo |
||
Halmashauri ya Wilaya ya Meru |
Maroroni |
||
Halmashauri ya Wilaya ya Meru |
Leguruki |
||
Halmashauri ya Wilaya ya Meru |
Makiba |
||
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli |
Moita |
||
2. 2 |
DAR ES SALAAM |
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni |
Mbweni |
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke |
Kijichi |
||
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo |
Saranga |
||
3. |
DODOMA |
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa |
Chipogolo |
4. |
GEITA |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale |
Bukwimba |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita |
Senga |
||
5. |
IRINGA |
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa |
Kitwiru |
Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo |
Kimala |
||
6. |
KILIMANJARO |
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi |
Bomambuzi |
Halmashauri ya Wilaya ya Hai |
Mnadani |
||
Halmashauri ya Wilaya ya Hai |
Machame Magharibi |
||
Halmashauri ya Wilaya ya Hai |
Weruweru |
||
7. |
LINDI |
Halmashauri ya Manispaa ya Lindi |
Chikonji |
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa |
Mnacho |
||
8. |
MANYARA |
Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ |
Nangwa |
9. |
MBEYA |
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe |
Ibighi |
10. |
MOROGORO |
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro |
Kiloka |
Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi |
Sofi |
||
11. |
MTWARA |
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba |
Milongodi |
Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani |
Reli |
||
Halmashauri ya Mji wa Masasi |
Chanikanguo |
||
12. |
MWANZA |
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi |
Kijima |
Halmashauri ya Jiji la Mwanza |
Mhandu |
||
13. |
RUKWA |
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga |
Sumbawanga |
14. 14 |
RUVUMA |
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru |
Lukumbule |