Home » Nje Ya Afrika » Madaktari wasiokuwa na mipaka ya MSF, wametangaza kutochukua fedha zozote kutoka kwa Umoja wa Ulaya.

Madaktari wasiokuwa na mipaka ya MSF, wametangaza kutochukua fedha zozote kutoka kwa Umoja wa Ulaya.

17 June 2016 | Nje ya Afrika

Madaktari wasiokuwa na mipaka ya MSF, wametangaza kutochukua fedha zozote kutoka kwa Umoja wa Ulaya.

Shirika la Madaktari hao wamesema sababu yao ya kuchukua uamuzi huo ni kwa sababu ya sera mpya ya Umoja huo kuhusu wakimbizi.

MSF inasema, mkataba wake na Uturuki kuwa nchi hiyo iwachukue wakimbizi wote watkaofikia Ugiriki haukubaliki.

Mwaka uliopita, Shirika hilo lilipokea Dola Milioni 63 kutoka kwa Umoja huo kuwasaidia wakimbizi hao.

Madaktari hao wanasema, sera hiyo ni ya ubaguzi na kuwafanya wkaimbizi hao ambao wengi wanayakimbia makwao kama Syria kwa sababu ya vita na kukimbilia maeneo salama ya Ulaya.

Aidha wanasema, sera hiyo inapunguza uwezekano wa kuendelea kuwasaidia wakimbizi hao.

Mataifa mengi ya Umoja wa Ulaya yamekuwa yakilalamikia ongezeko la wakimbizi katika nchi zao, idadi ambayo mwishi ilishuhdiwa wakati wa vita vya dunia vya pili.

 

Ad