Shutuma kuhusu shambulizi baya la anga kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao kaskazini mwa Syria
Shutuma kuhusu shambulizi baya la anga kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao kaskazini mwa Syria zimeongezeka leo Ijumaa wakati serikali ikikanusha kuhusika, wakati huohuo mpango tete wa kusitisha mapigano ukitekelezwa katika uwanja wa vita mjini Aleppo.
Wanawake na watoto wameripotiwa kuwa miongoni mwa raia 28 waliouawa katika mashambulizi ya Alhamisi karibu na mpaka wa Uturuki, ambayo yalijeruhi watu wengine 50.
Mashambulizi ya anga katika jimbo la Idlib, ambalo linadhibitiwa na waasi wa Al-Nusra Front ambao ni washirika wa waasi Al Qaaeda nchini Syria, yametekelezwa saa 48 baada ya kutekelezwa kwa mpango wa kusitisha mapigano katika mji wa Aleppo hadi mashariki.
Mpango wa kusitisha mapigano ni sehemu ya juhudi za kimataifa za kufufua makubaliano ya kihistoria ya mwezi Februari kuhusu kusitisha mapigano na zinafanya mazungumzo ya amani ili kumaliza miaka mitano vita ambayo yameua zaidi ya watu 270,000 na mamilioni kukimbia makazi yao.