Home » Afrika » Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC inasema haijiuzulu

Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC inasema haijiuzulu

05 May 2016 | Afrika

Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC inasema haijiuzulu licha ya kuendelea kupata shinikizo kutoka kwa wanasiasa wa upinzani kuelekea uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Makamishena wa Tume hiyo wanasema, wao sio mafisadi na wala hawaegemei upande mmoja kama inavyodaiwa na muungano wa CORD.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Isaak Hassan akizungumza leo na wanahabari jijini Nairobi amesema, wako tayari kukutana na wadau wote kujadili maswala yanayolalamikiwa na wao hawawezi kujiuzulu kwa sababu hawana kosa na wanaendelea na maandalizi ya uchaguzi wa mwakani.

Wanasiasa wa upinzani wanatishia kutoshiriki katika uchaguzi wa mwakani ikiwa tume hiyo haiatafanyiwa marekebisho na jana walizundua vuguvugu linalofahamika kwa jina la Firimbi Movement kupiga kambi kila Jumanne katika Makao Makuu ya Tume hiyo kuendelea kushikiza kujizulu kwa Makamishena hao.

 

Ad