Kizza Besigye asitangazwe LIVE
Serikali ya Uganda imepiga marufuku vyombo vya Habari nchini humo kupeperusha matangazo ya moja kwa moja maandamano ya upinzani yakiongozwa na Kizza Besigye kutoka chama cha FDC kuendelea kupinga ushindi wa rais Museveni mwezi Februari.
Hii inamaanisha kuwa vyombo vya Habari haviruhusiwi kuwahoji wanasiasa wa upinzani au kuonesha shughuli zao za kisiasa wakati huu rais Museveni akitarajiwa kuapishwa Alhamisi ijayo.
Besigye ameendelea kudai kuwa alishinda uchaguzi uliopita, ametangaza kuongoza maandamano dhidi ya rais Museveni lakini pia kusema ataapishwa sambamba na rais Museveni, shughuli ambazo zimezuiwa na Mahakama.
Jenerali Jim Muhwezi ni Waziri wa Habari anasema, vyombo vya Habari vutakavyokwenda kinyume na marufuku haya, vitachukuliwa hatua.