Chama cha kansela wa Ujerumani, Angela Merkel kimepata pigo
Chama cha kansela wa Ujerumani, Angela Merkel kimepata pigo kubwa kwenye uchaguzi wa majimbo uliofanyika hapo jana, ambapo wachambuzi wa mambo wanasema hali hiyo imetokana na sera ya chama chake kuhusu wahamiaji na wakimbizi.
Chama cha mrengo wa kulia cha AFD kimeshuhudiwa kikiweka historia kwenye uchaguzi wa safari hii, baada ya kupata kura nyingi zinazoelezwa kutoka kwa wananchi wenye hasira na sera za Kansela Merkel kuhusu wahamiaji.
Chama cha Christian Democratic Union CDU kimeshindwa kwenye majimbo mawili kati ya matatu, ambapo kimeambulia asilimia 27 kwenye ngome yake ya mjini Baden Vutembeg ambako kilishika nafasi ya pili.
Chama cha AFD ambacho sera zake ni za msimamo mkali, hivi karibuni kilidai kuwa ikiwa kitaingia madarakani, kitaruhusu polisi kutumia risasi za moto kukabiliana na wahamiaji wanaotaka kuingia nchini humo.