Staffan de Mistura amepongeza maendeleo ya usitishwaji mapigano
04 March 2016 | Nje ya Afrika
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria Staffan de Mistura amepongeza maendeleo ya usitishwaji mapigano, lakii hata hivyo amesema hakuna dhamana ya hali hiyo kuendelea.
Hata hivyo Demistura amesema hali ilivyo kwenye uwanja wa mapambano ni tulivu, lakini ni dhaifu, hivyo hakuna dhamana ya utulivu huo kuendelea kushuhudiwa. Vikao vinaendelea kuhakikisha pande zote mbili zinaendelea kuhsimisha makubaliano.
Katika hatuwa nyingine, waziri mkuu wa Uingereza David Cameron atajadiliana hapo kesho kwa njia ya sim na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, rais wa Ufaranss Francois Hollande pamoja na rais wa Urusi Vldimir Poutine kuendelea kuchochea makubaliano ya usitishwaji mapigano.