Marais EAC wasaini ya Kanuni za Madili ya Mfuko wa Sekta Binafsi
Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamemteuwa rais wa Tanzania John pombe Magufuli kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya hiyo katika mkutano wa 17 wa marais uliofanyika hii leo huko Arumeru Mkoani Arusha.
Akihutubia katika mkutano huo rais magufuli amesema viongozi wa Jumuiya hiyo wote kwa pamoja wamekubali ombi la Sudani Kusini kujiunga na Jumuiya hiyo.
Aidha rais Magufuli amesema Viongozi wa nchi wanachama wameridhia kwa pamoja ombi hilo la Sudani baada ya baraza la mawaziri kuridhia pia ombi hilo la Sudani Kusini iliomba kujiunga sasa ni miaka mitano.
Akipewa nafasi ya kuhutubia muda mfupi baada ya nchi yake kukubaliwa kuwa nchi mwanachama wa Jumuiya hiyo makam wa rais James Waniiga amepongeza hatuwa iliofika ambayo amesema itakuwa na manufaa makubwa kwa nchi yake.
wakati akihitimisha mkutano huo rais Magufuli amewataka viongozi wa sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya kazi.
Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda akijiandaa kuweka saini ya Kanuni za Madili ya Mfuko wa Sekta Binafsi wakati wa Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha
Rais Paul Kagama wa Rwanda akiweka saini ya Kanuni za Madili ya Mfuko wa Sekta Binafsi wakati wa Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiweka saini ya Kanuni za Madili ya Mfuko wa Sekta Binafsi wakati wa Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha
Wanafunzi walioshinda mashindano ya Insha ya EAC wakipata selfie na viongozi baada ya Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Mashariki jijini Arusha