Ban Ki Moon ametembelea kambi za watu waliokimbia makazi yao mashariki mwa DRC
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametembelea kambi za watu waliokimbia makazi yao mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC na kueleza hatua ambazo Umoja wa Mataifa utachukua kukabiliana na hali hiyo.
Ban Ki Moon amesema kuwa matatizo yanayowakumba raia wa mashariki mwa DRC yanapaswa kutfutiwa ufumbuzi kwa kuzingatia haki za binadamu na kuepusha mauaji ya mara kwa mara.
Ziara Ban Ki Moon inakuja wakati huu Umoja wa Mataifa ukisema kuwa kuna mpaka kufikia mwezi Septemba mwaka jana idadi ya watu waliokimbia makazi yao imefikia watu milioni moja nukta sita huku jimbo lakivu Kaskazini Likiathirika zaidi.
NCHI ya jamhuri ya kidemokrasia imekuwa ikikabiliwa na mapigano yanayoelezewa kuwa ya kikabila na ardhi kwa kipindi cha miaka 20 sasa.