Home » Tanzania » Tanzania Kuanzisha kitengo cha uhalifu wa wanyama pori kupambana na ujangili

Tanzania Kuanzisha kitengo cha uhalifu wa wanyama pori kupambana na ujangili

10 February 2016 | Tanzania

Waziri wa Mali asili na Utalii wa Tanzania Profesa Jumanne Maghembe amesema Tanzania imepanga kuanzisha Kitengo maalumu cha kukabiliana na uhalifu wa Wanyamapori ikiwa kwenye juhudi ya kuzidisha mapambano yake dhidi ya ujangili.

Hatua hiyo imekuja siku chache tu tangu majangili waitungue helikopta iliyokuwa kwenye doria ya kawaida katika Hifadhi ya Maswa iliyopo kusini mwa Mbuga ya Taifa ya Serengeti, na kumuua rubani ambaye ni Muingereza Roger Gower. Katika tukio hilo hadi sasa wameshakamatwa watu tisa.

Kwa mujibu wa Profesa Maghembe kitengo hicho kitajumuisha wataalamu kutoka sehemu mbalimbali zikiwemo Mamlaka ya Wanyapori ya Tanzania, Mbuga za wanyama za Tanzania, huduma za misitu pamoja na taasisi za Hifadhi za ndani na nje.

Ad