Home » Nje Ya Afrika » India: Wanafunzi Watanzania wahofia usalama wao

India: Wanafunzi Watanzania wahofia usalama wao

05 February 2016 | Nje ya Afrika

Licha ya serikali ya India kutangaza kuwa watu 5 wamekamatwa kwa kosa la kuwashambulia na kumvua nguo mwanafunzi mmoja raia wa Tanzania, hofu bado imetanda miongoni mwa takriban wanafunzi

150 wa chuo cha Acharya Kaskazini mwa Bangalore .

wawakilishi wa wanafunzi hao wameiambia BBC kuwa uoga na hofu ya kutokea kwa mashambulizi zaidi dhidi yao ndio imewafanya watanzania hao kukataa kutoka makwao wakihofia usalama wao.

Hata mkutano ulioitishwa na bodi inayosimamia chuo hicho cha Acharya haukuhudhuriwa na wanafunzi kutokana na tishio la usalama wao.

''Wanafunzi wachache mno walihudhuria mkutano huo kwani wengi wao wanaogopa wakitoka makwao wanweza kushambuliwa na wenyeji.

Wameamua kukaa ndani kufuatia mashambulizi hayo alisema rais wa wanafunzi raia wa Tanzania Bernandoo Kafumu.

Kundi la wenyeji walioshuhudia ajali hiyo walimshambulia na kulichoma moto gari hilo.

Kundi la wenyeji waliojawa na hasira bila ya kutaka kujua uraia wao waliwashambulia wasichana hao watanzania wakamvua nguo mmoja wao.

Gari lao lilikuwa tayari limechomwa moto.

Wanadai ilikuwa ni'' hasira tu ya barabarani''.

Vile vile polisi wanakanusha kuwa mwanafunzi huyo wa kike aliyevuliwa nguo ''hakudhulumiwa kimapenzi''

Kamishna wa Polisi wa jimbo hilo la Bangalore, N S Megharik, ameiambia BBC kuwa uchunguzi wa kisa hicho unaendelea.

Kamanda mkuu wa polisi katika jimbo la Karnataka, Om Prakash, amewaomba wanafunzi hao wajitokeze iliwakutane naye jambo ambalo wanafunzi hao wamelipinga wakisema hiyo itahatarisha maisha yao tu wakatu huu ambapo wanahisi bado kunahasira miongoni mwa wenyeji.

''Nataka nikueleze wazi hakuna vile tutaondoka makwetu kwenda kukutana na kiongozi wa polisi ama hata waziri anayesimamia jimbo hili la Karnataka kwa sababu hatuna ulinzi.

Chuo chetu kiko nje ya mji, kwa hivyo lazima tutapita vijijini ambako mahasidi wetu wapo'' alisema mwanafunzi huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Waziri wa usalama katika jimbo hilo ameiambia BBC kuwa doria ya polisi itaongezwa katika eneo hilo ilikulinda maisha yao.

Ad