Home » Afrika » Serikali ya Syria na Upande wa upinzi wamenyoosheana kidole mazungumzo

Serikali ya Syria na Upande wa upinzi wamenyoosheana kidole mazungumzo

04 February 2016 | Afrika

Serikali ya Syria na Upande wa upinzi wa syria wamenyoosheana kidole cha lawama kufuatia kusitishwa kwa mazungumzo ya amani ya huko Geneva.

Mjumbe wa umoja wa mataifa Staffan de Mistura ametoa wito wa kusitishwa kwa mazungumzo ya amani kuhusu syria kwa muda hadi yatakapoendelea tarehe 25 mwezi huu.

Hata hivyo wajumbe wa upinzani HNC wamesema hawatarejea katika meza ya mazungumzo hadi pale masharti yao yatakapokuwa yamezingatiwa nchini syria wakituhumu vikosi vya serikali kuendelea kushambulia raia.

Serikali ya Syria kwa upande wake imesema Upinzani ndio chanzo cha kusitishwa kwa mazungumzo ya amani wakifuata amri za Uturuki na mataifa ya ghuba ya kiarabu.

Hii leo alhamisi mkutano wa mataifa wahisani utafanyika London Uingereza kwa lengo la kufanya changizo la fedha kwa ajili ya wahanga wa vita.

 

Ad