Mahakama ya rufaa nchini Misri imebadilisha hukumu ya kunyonga Wafuasi wa Brotherhood
03 February 2016 | Afrika
Mahakama ya rufaa nchini Misri imebadilisha hukumu ya Mahakama kuu nchini humo iliyotaka wafuasi 149 wa kundi lillopigwa marufuku la Muslim Brotherhood kunyongwa .
Mahakama imetaka watu hao kushtakiwa upya kwa tuhma za kusababisha mauaji ya maafisa wa polisi 13 karibu na jiji kuu Cairo mwaka 2013.
Watu wengine, 37 walikuwa wamehukumiwa kifo na Mahakama ya rufaa imewataka kujisalimisha ili kufunguliwa upya mashtaka yanayowakabili.
Francis Wambete ni Mchambuzi wa siasa za Kimataifa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Makerere jijini Kampala nchini Uganda.