Umoja wa Mataifa wasisitiza haja ya kutimiza ahadi
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Ban Ki-moon amesema ahadi ya azimio la Umoja huo kwa watu walio kwenye hali duni inapaswa kuendelea kutimizwa.
Katibu huyo amesema mwaka wa 2015 ulikuwa ni mwaka wa migogoro, na kutolea mifano ya Syria ma Yemen. Alisema matukio kama hayo ambayo yanakiuka haki za kimsingi za kibinadamu ni kinyume na maazimio ya Umoja huo na ni changamoto kwa baraza la usalama kutimiza wajibu wake.
Naye mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw Liu Jieyi ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kulinda malengo na kanuni za maazimio ya Umoja huo. Amesema maazimio hayo yanatokana na maovu ya Vita Kuu ya Pili Duniani na hivyo yanatoa mwongozo wa jinsi watu wanavyopaswa kushirikiana kujenga dunia.