Home » Nje Ya Afrika » Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Mheshimiwa Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Mheshimiwa Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

19 April 2016 | Nje ya Afrika

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe ameapishwa leo tarehe 19 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.

Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Batilda Salha Burian ambaye Mkataba wake umemalizika.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa, Mheshimiwa Chikawe ameahidi utumishi uliotukuka na kuiunganisha vyema Tanzania na Japan hususani katika masuala ya kiuchumi.

Mheshimiwa Chikawe ametoa wito kwa watanzania wote hasa waishio Japan na nchi nyingine zinazotumia Ofisi ya Ubalozi huo wa Tanzania, kuutumia vizuri ubalozi huo ili kunufaika na fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji.

Ubalozi wa Tanzania nchini Japan, pia unatoa huduma za kibalozi katika nchi za Korea Kusini, New Zealand, Papua New Guinea na Australia.

 

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

19 Aprili, 2016

 

Ad