Rais Barack Obama, kufanya ziara ya kihistoria nchini Cuba.
14 March 2016 | Nje ya Afrika
Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye juma lijalo atafanya ziara ya kihistoria nchini Cuba, amewahakikisha raia wa nchi hiyo wanaoishi ughaibuni, kuwa atatumia ziara hiyo kujadili masuala ya haki za binadamu na utawala wa Havana.
Kwenye barua iliyocahpishwa mwishoni mwa juma kwa wanaharakati wanawake wa Cuba wanaoishi nchini Marekani, rais Obama, amesema suala kuu ambalo atajadiliana na mwenzake rais Raul Castro ni kuhusu masuala ya haki za binadamu.
Rais Obama kwenye barua yake, amesema anafahamu vikwazo vilivyoko nchini Cuba na hasa vinavyowakabili wafungwa wa kisiasa, na kuongeza kuwa hakuna mt yeyote anayeishi nchini Cuba, anayepaswa kufanyiwa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu.