Home » Nje Ya Afrika » Nchi ya Marekani imetangaza kuwa hivi karibuni itafunga rasmi kituo chake cha kijeshi

Nchi ya Marekani imetangaza kuwa hivi karibuni itafunga rasmi kituo chake cha kijeshi

05 January 2016 | Nje ya Afrika

Nchi ya Marekani imetangaza kuwa hivi karibuni itafunga rasmi kituo chake cha kijeshi cha operesheni za ndege zisizo na rubani, kilichoko kusini mwa nchi ya Ethiopia.

Kituo hicho ambacho kipo umbali wa kilometa 400 kusini mwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, kimekuwa kikitumika toka mwaka 2011, kutekeleza mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa kijihadi kwenye pwani ya Afrika Mashariki.

Awali Marekani ilidai kuwa kituo hicho kilikuwa kinatumia ndege zisizo na rubani kufanya doria na kufuatilia mienendo ya makundi hayo, lakini baadae ikabainika kuwa imekuwa ikitekeleza mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa kiislamu wa Al-Shabab nchini Somalia.

Ad