Magaidi kuvuliwa uraia, yapitishwa na bunge la Ufaransa
10 February 2016 | Nje ya Afrika
Baraza la chini la bunge la Ufaransa limepitisha mswada wa marekebisho ya katiba yanayolenga kuwavua magaidi uraia wa Ufaransa.
Kwa mujibu wa mswada huo, adhabu hiyo ya ziada itatolewa kwa magaidi au wahalifu wanaokiuka maslahi ya kimsingi ya taifa.
Mtu anayechukuliwa hatua hiyo atanyang'anywa haki zote za kiraia zikiwemo haki ya kuchagua, kuchaguliwa na kufanya kazi kama mtumishi wa serikali.
Marekebisho hayo ya katiba yanalenga kutoa urahisi wa kuweka hali ya hatari. Hata hivyo, hatua hiyo imesababisha wasiwasi miongoni mwa baadhi ya watu kuhusu kudhoofisha haki na uhuru wa raia