Home » Nje Ya Afrika » Barack Obama kuchukua hatua kuhusu udhibiti wa silaha

Barack Obama kuchukua hatua kuhusu udhibiti wa silaha

05 January 2016 | Nje ya Afrika

Rais wa Marekani, Barack Obama hii leo anatarajiwa kutumia madaraka yake ya juu kuchukua hatua kuhusu udhibiti wa silaha, akiacha kutumia bunge la Congress, hatua inayoashiria kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa mgumu kwa chama chake.

Mwaka uliopita rais Obama alionesha waziwazi kitofautiana na wanasiasa wanaopinga mapendekezo yake, ambapo aliahidi kutumia madaraka ya rais, hatua inayopuuzilia mbali upinzani wa bunge la Congreaa dhidi ya mapendekezo yake.

Mwanasheria mkuu wa Serikali ya Marekani, Loretta Lynch, amesema kuwa hatua hizi zinazochukuliwa na rais Obama, zitaweka mipaka na sheria kali kuhusu wauzaji wa silaha, na kuruhusu uhakiki wa taarifa za wanunuzi wa silaha zenyewe.

Baadae hii leo rais Obama atalihutubia taifa kueleza azma yake, wakati huu tayari wabunge wa Republican, watengeneza silaha na watumiaji wake wakikashifu hatua yake.

Ad