BALOZI MIGIRO AMTUNUKU KIJANA ALIYESHINDA PICHA ZA KIMATAIFA
20 June 2017 | Nje ya Afrika
Baadhi yetu huwaita wenye hali hii “taahira” – neno la asili ya Kiarabu lenye maana “mtu asiye sawa” (wazimu, chizi, bwege, nk). Sahihi ni “mtindio ubongo” – kwa Kiingereza “Down Syndrome”....
Baadhi ya taswira zake ni : kufikiri na kuzungumza taratibu, kigugumizi, mwili mfupi, utofauti wa tambo la kichwa,vidole vya mikono na miguu,nk.
Mwaka huu kijana wa miaka 18, Samwel Mwanyika, mwenye “Mtindio Ubongo “ (Down Syndrome) alikuwa mshindi wa kimataifa wa upigaji picha.
Balozi wetu Uingereza Mheshimiwa Asha-RoseMigiro akaeleza:
“Wametoka vijana wengi kwenye nchi zilizoendelea, wengine wamemzidi umri...tena wenzetu huwa na mipango maalum ya kuwapa mbinu mbalimbali,...sasa huyu wa familia ya kawaida tu ya Kitanzania ambapo bado hatujaweka miundo mbinu kama walivyoweka huku, picha yake imeshinda...”
Mwasisi wa kujitolea wa shirika la Mtindio Ubongo (Pearl of People with Down Syndrome) , Mony Teri Pettite na wazazi wake Samwel, Philip Mwanyika na Sophie Mshangama, walikutana na Balozi Migiro na kupongezwa Ijumaa iliyopita. Afisa Utawala Ubalozini, Rose Kitandula , pia alikuwepo.Picha na Habari za Freddy Macha
Samwel Mwanyika na picha iliyonyakua tuzo la kimataifa la Stephen Thomas, mjini London.
Balozi Migiro akimvika Samwel Mwanyika bendera ya taifa, alipowakaribisha na familia ofisini kwake, Ijumaa 16, Juni 2017.
Balozi Migiro, na Afisa Utawala Ubalozi London wakiwa na Samwel Mwanyika na mwenzake mwenye “Mtindio Ubongo” (Down Syndrome), Penina Haika Petitte.
Picha ya pamoja. Toka kushoto, Mjomba wake Sam, Hassan Mshangama, Mama Sam, Sophie Mshangama, Mony Teri Pettite, Penina Haika Pettite, Balozi Migiro, Sam Mwanyika, Rosa Kitandula (Afisa Utawala Ubalozini), na Philip Mwanyika (Baba wa mshindi).
Balozi Migiro akiwasikiliza wageni na kuwapongeza.
Balozi Migiro akizungumza na Mony Teri Petitte mwasisi wa “Pearl of People with DownSyndrome” anayejitolea kuendesha Jumuiya ya Watanzania wenye Mtindio Ubongo .
Tuzo ya Stephen Thomas
Tuzo ya Stephen Thomas