Home » Michezo » Sepp Blatter kumshawishi rais Piere Nkurunziza kutowania urais kwa muhula wa tatu

Sepp Blatter kumshawishi rais Piere Nkurunziza kutowania urais kwa muhula wa tatu

21 April 2016 | Michezo

Rais wa zamani wa Shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter mwaka uliopita alijaribu kuwa mpatanishi katika mzozo wa Burundi kumshawishi rais Piere Nkurunziza kutowania urais kwa muhula wa tatu, lakini hakufanikiwa.

Hili nimebainika baada ya kuzinduliwa kwa kitabu kumhusu Blatter.

Blatter ameeleza katika kitabu hiki kuwa Wizara ya Mambo ya nje ya Uswizi ilimwomba kuwa msuluhishi wa mgogoro.

Kiongozi huyo wa zamani wa soka anasema alizungumza na rais Piere Nkurunziza ambaye amemwelezea kama mtu anayependa sana mchezo wa soka, aachane na mpango wake wa kuwania tena urais na baadaye FIFA itampa kazi ya kuwa Balozi wa mchezo wa soka barani Afrika au duniani.

Katika kitabu hiki, Blatter anasema alitaka kutumia mchezo wa soka kusaidia kutatu mzozo wa Burundi na kuepuka machafuko ambayo yameendelea kushuhudiwa nchini humo.

Blatter anasema, rais Nkurunziza alimjibu kuwa ameguswa mno lakini akataa kukubali ombi lake.

Wizara ya Mambo ya nje ya Uswizi imekiri ni kweli ilikuwa na mkataba na Blatter kumtaka kutumia mchezo wa soka kuleta utulivu nchini Burundi lakini inasisitiza kuwa haikumaanisha rais Piere Nkurunziza asiwanie tena urais.

Ad