Mohamed Ali kuzikwa Ijumaa
Dunia imealikwa kuhudhuria msiba wa Muhammad Ali, kwenye mji alikozaliwa siku ya Ijumaa ambako maisha ya nguli huyu wa masumbwi yatasherehekewa huku uma ukipewa nafasi ya kushiriki mazishi na ibada ya kumbukumbu, amesema msemaji wa familia ya Ali.
Muhammad Ali, bingwa mara tatu wa uzito wa juu duniani na mwanaharakati wa haki za binadamu ambaye alikuwa nembo muhimu katika karne ya 20, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 74 kutokana na matatizo ya kiafya yaliyochangiwa kwa muda mrefu na mapambano yake dhidi ya ukongwa wa kutetemeka "Parkinson.
Taarifa rasmi kuhusu sababu za kifo cha Muhammad Ali, imeeleza kuwa alifariki kutokana na kupata mstuko, kitaalamu inafahamika kama "Septic Shock" ambapo hata hivyo kilichosababisha mshtuko huo hakijabainishwa kitaalamu.
Mwanamasumbwi huyo aliyekuwa na mbwembwe na uwezo mkubwa uliongoni, na ambaye matamshi yake yalikuwa yanawagusa wengi, yalikuwa hatari kama ngumi alizokuwa akizirusha uliongoni, ambapo alikimbizwa kwenye hospitali ya Arizona mwanzoni mwa wiki iliyopita.
Wanasiasa maarufu, wanamichezo, watu maarufu na mashabiki duniani kotea walisimama kwa dakika moja kumkumba "Bingwa" ambaye maisha yake yameduni kwa miongo mitatu.
Siku ya Jumapili familia ya Ali na ndugu wa karibu, waliusinidika mwili wake kutoka Arizona kwenda Louisville alikozaliwa kusini mwa jimbo la Kentucky.
Baada ya shughuli binafsi ya kifamilia Alhamisi ya wiki hii, jeneza la Ali litapitishwa kwenye mitaa ya Louisville siku ya Ijumaa, kabla ya kufanyika ibada maalumu ambayo watu wote wamealikwa itakayofanyika kwenye uwanja maalumu, ambapo rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton anatarajiwa kusoma wasifu wa Muhammad Ali.
Msemaji wa familia ya Ali, Bob Gunnell amewaambia waandishi wa habari kuwa, utaratibu wa mwili wa Ali kuwekwa kwenye uwanja mkubwa unalenga kutoa fursa kwa kila mtu atakayeshiriki kutoa heshima za mwisho kwa nguli huyu wa masumbwi.
Bendera kwenye mji wa Louisville zinapepea nusu mlingoti kwa heshima ya Ali, wakati huu mashabiki wake wakifurika kwa wingi kwenye makazi ya zamani aliyokuwa akiishi Ali ambayo sasa yamegeuzwa kuwa eneo la makumbusho, kutoa heshima zao.
"Mioyo yetu imeumia sana. Lakini tunafuraha kwakuwa baba yuko huru sasa," alisema mtoto mkubwa wa Muhammad Ali, Hana Ali kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter.
Rais wa Marekani, Barack Obama alitoa pole kwa familia kwa mtindo ambao haukuwa wa kawaida, kwakuwa alimzungumzia Ali, kwa yeye binafsi kama alivyomfahamu na kwamba anazitunza kwenye chumba chake binafsi, pea mbili za Gloves alizokuwa akizivaa, Muhammada Ali.
"Muhammad Ali alikuwa bingwa wa mabingwa, huo ndio ukweli," alisema rais Obama.
"Mapambano yake nje ya ulingo yalimgharimu mikanda yake na imani kwa uma. Ingeweza kumtengenezea maadui, kushoto na kulia na hata kukaribia kuswekwa jela, lakini Ali alisimamia kile alichoamini," aliongeza rais Obama.
Katika hali ya kawaida kabisa, Bill Clinton ambaye atasema neno kuhusu Ali wakati wa ibada ya mazishi, yeye pamoja na mke wake Hillary anayewania kuteuliwa na chama chake kuwania urais wa Marekani, wamesema Ali, alikuwa kiungo muhimu cha uzuri na baraka, kasi na nguvu ambavyo kamwe haviwezi kulinganishwa,"
Ali alipelekwa hospitali ya Phoenix mwanzoni mwa juma, lakini hali yake ilibadilika ghafla na kuanza kuzorota.
Muda wake wa mwisho, Ali aliutumia akiwa amezungukwa na familia yake na kwamba hakuumia.
Ali amekuwa akiishi kwenye mji wa Phoenix na mkewe Lonnie, akiwa ni mke wa nne aliyemuoa mwaka 1986, alifanikiwa kuwa na wajukuu tisa, watoto wakike saba na wawili wa kiume.
Msemaji wa familia ya Ali, amesema kuwa bindio huyo kwa sehemu kubwa ndiye aliepanga utaratibu wa namna atakavyombolezwa.
Kwa hisani ya RFI Kiswahili