YALIYOJIRI BUNGENI KATIKA KIPINDI CHA MASWALI NA MAJIBU - SEPTEMBA 13, 2017.
#WizarayaAfya hadi sasa imesambaza vifungashio 60,000 kwa mikoa 6 ya kanda ya Ziwa - Dkt. Hamisi Kigwangala.
#Ni jukumu la kila Halmashauri kuweka mahitaji ya vifungashio (delivery pack) - Dkt. Hamisi Kigwangala.
#Wizara imepata ufadhili wa Bil. 66 kutoka Benki ya Dunia ambapo itaboresha vituo 100 - Dkt. Hamisi Kigwangala.
#Vituo hivyo vitaboreshwa ili kutoa huduma za dharura za upasuaji wa kutoa mtoto - Dkt. Kigwangala.
#Fedha za utekekezaji zimeanza kupelekwa katika Halmashauri husika - Dkt. Hamisi Kigwangala.
#Wizara ya Afya imewaandikia barua Wizara ya Fedha kuona namna ya kuondoa kodi kwa taulo za kike - Dkt. Hamisi Kigwangalla.
#Majadiliano yanaendelea ili kuwezesha bidhaa hii kuunganishwa katika orodha ya vifaa tiba - Dkt. Hamisi Kigwangala.
#Kuna wanafunzi wanakosa masomo hadi siku tano kutokana na kukosa vifaa hivyo - Mhe. Ummy Mwalimu.
# Wapo mabinti wanaotumia majani kujisitiri kutokana na kukosa taulo hizo - Ummy Mwalimu.
#Makusanyo yatokanayo na kodi za majengo kutoka Halmashauri, Manispaa na Majiji yameongezeka - Dkt. Ashatu Kijaji.
#Makusanyo hayo yameongezeka kutoka Bil. 28.28 mwaka 2015/16 mpaka Bil. 34.09 mwaka - 2016/17 - Dkt. Ashatu Kijaji.
#Makusanyo ya mwaka 2015/16 yalikusanywa na Serikali za mitaa na mwaka 2016/17 TRA ilianza kukusanya kodi hiyo - Dkt. Ashatu Kijaji.
#Ongezeko hilo ni sawa na 20.6% ya makusanyo ya Halmashauri husika kabla ya kodi hiyo kuhamishiwa TRA - Ashatu Kijaji.
#Serikali imeanza kutekeleza mpango wa TBC wa kujenga mitambo ya FM nchi nzima - Mhe. Anastazia Wambura.
#Serikali kupitia mradi unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa Mkopo wa masharti nafuu imeendelea na maandalizi ya ujenzi wa Chuo kipya cha ufundi stadi cha Mkoa wa Simiyu - Eng. Stella Manyanya.
Imeandaliwa na Idara ya Habari - MAELEZO.