Serikali imeuza TANI LAKI 1 kati ya tani laki mbili na nusu ilizonunua kutoka kwa wakulima kwenye Oparesheni Korosho.
Serikali imeuza TANI LAKI 1 kati ya tani laki mbili na nusu ilizonunua kutoka kwa wakulima kwenye Oparesheni Korosho.
Mnunuzi amekubali kununua tani zote hizo kwa bei ya Tsh. 4,480 kwa kilo moja sawa na zaidi ya Tsh. Bilioni 410.
Kampuni iliyosaini mkataba wa kununua korosho ghafi imekubali kulipa ushuru na kuicha serikali ikikusanya faida ya Tsh. Bilioni 150 baada ya kununua kwa Tsh. 3,300 kwa kila kilo kutoka kwa wakulima.
Malipo yote baada ya makubaliano hayo kufanyika ndani ya WIKI MOJA baada ya tarehe ya kusaidi mkataba ambao umesainiwa siku ya Jumatano tarehe 30 Januari, 2018 jijini Arusha.
Makubaliano ya kuuza korosho hizo yaliongozwa na Waziri wa Sheria na Katika Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi, Waziri na Naibu Waziri wa Kilimo, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.
Balozi na Maafisa wa Ubalozi wa Kenya nchini na viongozi wengine waandamizi wa serikali wanaohusika na biashara, kilimo, mahusiano ya kimataifa na sheria.