Home » Afrika » Zuma amesema uchunguzi kuhusu ununuzi wa silaha haukuwa na ufisadi

Zuma amesema uchunguzi kuhusu ununuzi wa silaha haukuwa na ufisadi

21 April 2016 | Afrika

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema uchunguzi kuhusu ununuzi wa silaha miaka ya tisini uliofanywa na serikali, umebaini kuwa haukuwa na visa vyovyote vya ufisadi.

Wapinzani wa serikali ya ANC kwa muda mrefu wamekuwa wakidai kuwa Dola Bilioni 2 nukta 1 zilizotumiwa na serikali kununua silaha hizo kununua silaha hizo kutoka jeshi kutoka Mataifa ya Ulaya, zilitumiwa vibaya na kwa sababu za kisiasa.

Rais Zuma amesema uchunguzi wa kibinafasi uliofanyika na tume ya ufisadi nchini humo umebaini kuwa hakuna ushahidi wowote uliopatikana kuhusu wizi wa fedha za umma kama ilivyodaiwa.

Mwaka 2005, aliyekuwa mshauri katika Wizara ya fedha Schabir Shaik, alipatiaka na kosa na kufungwa jela kwa kuomba rushwa ili kupata kandarasi ya kununua silaha kutoka kwa kampunzi moja ya Ifransa.

Hatua hiyo pia ilisababisha rais wa kipindi hicho Thambo Mbeki kumfuta kazi Zuma ambaye alikuwa ni naibu wake lakini baadaye mwaka 2009 Zuma akaondolewa tuhma hizo.

Wapinzani wamekuwa wakidai kuwa rais Zuma aliahidi kuilinda kampuni hiyo ya silaha baada ya kumalizika kwa ununuzi wa silaha hizo.

Rais Zuma amesema ripoti ya uchunguzi huo itawekwa wazi kwa umma hivi karibuni.

 

Ad