Viongozi wa Umoja wa Afrika kuwasili nchini Burundi hiyo kesho
24 February 2016 | Afrika
Viongozi wa Umoja wa Afrika wanatarajiwa kuwasili nchini Burundi hiyo kesho kama njia ya kuongeza jitihada za kumaliza mgogoro wa Burundi uliozuka mwezi April mwaka jana baada ya rais Pierre Nkurunziza kugombea urais kwa muhula wa tatu.
Ujumbe wa Umoja wa Afrika unaongozwa na rais wa Afrika Kusini Jakob Zuma na utakuwa nchini Burundi kwa siku mbili katika harakati hizo za kusaka amani nchini Burundi.
Viongozi wengine waliopo katika ujumbe huo ni
Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz,
Rais wa Senegal Macky Sall,
Rais Ali Bongo wa Gabon na
waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn.