MONUSCO wamethibitisha kuwa Majeshi yao yameimarisha ulinzi
28 January 2016 | Afrika
Maafisa wakuu wa jeshi la umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo MONUSCO wamethibitisha kuwa Majeshi yao yameimarisha ulinzi katika eneo la mpaka kati ya DRC na Burundi, majuma kadhaa baada ya kuenea kwa taarifa ya uwepo wa makundi ya waasi kutoka burundi katika eneo hilo.
Katika mahojiano na mwandishi wa RFI idhaa ya kifaransa Sonia Rolley aliyeko mjini Kinshasa, msemaji wa Monusco Prosper-Felix Basse amesema kuwa wanajeshi wa monusco watalisaidia jeshi la congo FARDC Katika shughuli zao za kupiga doria katika eneo hilo, na si vingionevyo.