Home » Afrika » Mahakama ya kijeshi imeanza kusikiliza kesi ya Germain Katanga

Mahakama ya kijeshi imeanza kusikiliza kesi ya Germain Katanga

03 February 2016 | Afrika

Mahakama ya kijeshi mjini kinshasa huko jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeanza kusikiliza kesi inayomkabili  aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi la FRPI , Germain Katanga al maarufu Simba kufuatia mauaji yaliyotekelezwa na kundi lake mwaka 2003 kijijini Bogoro nchini DRC.

Katanga mwenye umri wa miaka 38, alikamatwa mwezi Machi kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikiwemo mauaji na unyang'anyi, na kwa kushiriki katika mashambulizi ya kijiji cha Bogoro Mashariki mwa DRC mnamo Februari 24, 2003.

January 18 mwaka huu serikali ya kINSHASA ilisema haitamuachia huru Bwana Germain Katanga, baada ya kumaliza kutumikia hukumu aliyopewa na Mahakama ya Kimataifa ya ICC, naye alirejeshwa mjini Kinshasa nchini DRC mwezi desemba ili kumaliza wiki chache zilizokuwa zimebaki za kifungo chake.
Tinanzabo Zeremaya, ni m'bunge wa bunge la kitaifa na mmoja wa wanasiasa wenye umaarufu huko Bunia Wilayani Ituri alikokamatwa Germain Katanga na hapa anazungumza nasi akiwa Kinshasa, kuutoa mtazamo wake.

Ifahamike kuwa Mwaka 2014, ICC ilimhukumu Bwana Germain Katanga kifungo cha miaka 12 jela na ICC baada ya kumpata na hatia ya kutenda uhalifu wa kivita na jinai dhidi ya binadamu.

 

Ad