Home » Washirika » TTCL yazindua kampeni ya “NJOO NYUMBANI HUKO ULIKO SIO KWENU”

TTCL yazindua kampeni ya “NJOO NYUMBANI HUKO ULIKO SIO KWENU”

13 April 2017 | Washirika

TTCL yazindua kampeni ya “NJOO NYUMBANI HUKO ULIKO SIO KWENU"

Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imezindua kampeni  mpya ya kuhamasisha watumiaji wa simu za mkononi kujiunga na mtandao wa TTCL ulio boreshwa kwa kasi ya 4G LTE wakiwa na kauli mbiu ya ‘Njoo Nyumbani Huko uliko sio kwetu’.

Mteja atakapo nunua kifurushi chochote cha TTCL anapata BURE huduma za mitandao ya kijamii kama Whatsapp, facebook, twitter, Instergram na E-mail.

Kampeni hiyo imezinduliwa Katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na inatarajiwa kufanyika nchi nzima, TTCL imeboresha usikivu na huduma za kimtandao. Wakati wa kampeni hizi TTCL inatarajia kusajili wateja wapya wa simu za mkononi na watumiaji wa data.

Vifurushi vinavyopatikana sasa bei ni Nafuu ni Jiachie, Usipitwe, T-Connect, Bando la kijanja na Bando la Serereka.

Baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa hayana huduma za data laikini TTCL imeshafunga mitambo yake ni Katika Mbuga za wanyama ambako huduma hii inapatikana kwa SATELLITE BROADBAND.

 

 

Kauli mbiu “Karibu Katika kizazi cha T. Tumekufikia”