Home » Tanzania » Watanzania waungana katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani

Watanzania waungana katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani

01 May 2017 | Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo May 1, 2017 amehutubia kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani inayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Ushirika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Kila ifikapo May 1 kila mwaka Dunia huadhimisha Siku ya Wafanyakazi ikiwa ni kutambua, kuthamini, kujali na kuheshimu mchango wao katika maendeleo ya Dunia kwa ujumla ambapo katika kuiadhimisha siku hii Tanzania imekuwa na kauli mbiu inayosema: ‘Uchumi wa Viwanda uzingatie  Haki, Maslahi na Heshima kwa Wafanyakazi’.

Ad