Home » Tanzania » TOA maoni na ushauri kuhusu maboresho ya rasimu wa mpango kazi

TOA maoni na ushauri kuhusu maboresho ya rasimu wa mpango kazi

05 September 2016 | Tanzania
 
SERIKALI imeanza kupokea maoni na ushauri kutoka kwa asasi za kiraia, sekta binafsi na wananchi kuhusu maboresho ya rasimu wa mpango kazi wa kitaifa wa uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa uwazi wa Awamu ya tatu (2016/17 -2017/18).
 
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Susan Mlawi Ilisema mwisho wa kuwasilisha maoni na ushauri huo ni tarehe 10 Septemba mwaka huu saa 9:30 alasiri.
 
Mlawi alisema mpango kazi huo utahusisha vipaumbele katika maeneo saba ambayo ni pamoja na upataji taarifa, takwimu huria, bajeti za wazi, uwazi kuhusu ardhi, uwazi kuhusu tasnia ya uziduaji, uwazi katika masuala ya afya, na mifumo ya utendaji kazi.
 
Aidha aliongeza kuwa maoni, ushauri na mapendekezo hayo yanaweza kuwasilisha Serikalini katika njia mbalimbali za mawasiliano ikiwemo  
tovuti rasmi ya wananchi
 
tovuti ya ogp
 
government open data portal
 
 Mlawi alizitaja njia nyingine za kuwasilisha maoni hayo ni katika barua pepe ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma
 
pamoja na njia ya barua kupitia
sanduku la posta
S.L.P 2483
Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa Mlawi alisema rasimu ya mpango kazi inapatikana katika tovuti  ya wananchi
tovuti ya ogp
government open data portal
tovuti ya ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma
pamoja na mitandao ya kijamii ya facebook (utumishi week) na
blog
 
“Moja ya vigezo na matakwa ya utekelezaji wa mpango huu kwa nchi mwanachama ni kuandaa mpango kazi wa kitaifa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo Asasi za kiraia, sekta binafsi na wananchi, hivyo Serikali inawahimiza wadau kushiriki kikamilifu kutoa maoni yao” alisema Mlawi.
 
Mpango wa uendeshaji wa Serikali kwa uwazi ni jitihada za kimataifa katika kuhimiza uendeshaji wa Serikali kwa uwazi zaidi, ushirikishwaji mkubwa wa wananchi, kudhibiti rushwa katika jamii na kuimarisha utoaji huduma bora kwa wananchi. Tanzania ilijiunga na mpango huo mwaka 2012.
 
 
 
Ad