Home » Tanzania » Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13 Desemba, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wote wa Tanzania Bara

Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13 Desemba, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wote wa Tanzania Bara

20 December 2018 | Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13 Desemba, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wote wa Tanzania Bara, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Huruma Mkuchika na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo.

Wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Adelardius Kilangi, Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Musa Iyombe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere.

Katika kikao hicho Mhe. Rais Magufuli na viongozi hao wa Mikoa wamezungumza masuala mbalimbali yanayohusu utendaji kazi wa Serikali mikoani hususani usimamizi wa shughuli za maendeleo na utoaji wa huduma kwa wananchi.

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

13 Desemba, 2018

Ad