Home » Tanzania » Rais Magufuli, amemteua Mwenyekiti wa (ATCL)

Rais Magufuli, amemteua Mwenyekiti wa (ATCL)

16 September 2016 | Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Mhandisi Emmanuel Korosso kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi Emmanuel Korosso unaanza mara moja.

Mhandisi Emmanuel Korosso anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Salim Msoma ambaye alimaliza muda wake.

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

15 Septemba, 2016

Ad