Home » Tanzania » Mradi wa Kidijitali kwa Shule za Msingi

Mradi wa Kidijitali kwa Shule za Msingi

14 March 2017 | Tanzania

Makamu wa Rais Samiah Suluhu Hassan amezindua mradi wa Kidijitali kwa Shule za Msingi katika Manispaa ya Dodoma wenye zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni mia nane unaokusudiwa kunufaisha takriban shule hamsini.

Akizungumza baada ya kuuzindua mradi huo mjini Dodoma, ambapo jumla ya wanafunzi elfu tano watakabidhiwa Ipad, Makamu wa Rais amesema mradi huo utasaidia juhudi za serikali katika kasi yake ya kuendea uchumi wa viwanda.

Ad