Home » Tanzania » MAGUFULI avipongeza vyombo vya ulinzi na usalama

MAGUFULI avipongeza vyombo vya ulinzi na usalama

16 November 2015 | Tanzania

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi- CCM, Dkt JOHN MAGUFULI amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri ya kuendeleza utulivu na amni nchini na kuahidi kuboresha maslahi yao zaidi mara baada ya kupata ridhaa ya kuingoza nchi.

Dkt. MAGUFULI ametoa pongeza hizo katika wilaya za MKINGA na BUMBULI mkoani TANGA katika muendelezo wa kampenzi zake za kusaka kura kwa wananchi wa mkoa wa TANGA.

Ahadi ya Dakta MAGUFULI kuhusu kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015/2020 inayotaja bayana katika kipindi cha miaka mitano serikali za CCM kuendelea kuimarisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama kwa kuviongezea rasilimali fedha,watu, maslahi ,zana za kisasa na mafunzo.

Dakta MAGUFULI pia ameahidi kujenga barabara ya kutoka SONI hadi BUMBULI kwa kiwango cha lami.

Aidha ameahidi kushughulikia mgogoro wa kiwanda cha KUSINDIKA chai cha MPONDE kilichopo BUMBULI ambacho kwa sasa hakifanyi kazi.

Dakta MAGUFULI amemaliza mikutano yake ya kampeni mkoani TANGA na kutarajiwa kuanza kufanya kampeni katika mkoa wa MARA.

Ad