Home » Tanzania » Jakaya Mrisho Kikwete Fundation (JMKF)

Jakaya Mrisho Kikwete Fundation (JMKF)

14 March 2017 | Tanzania

Rais mstaafu  Jakaya Kikwete amesema Taasisi ya Maendeleo ya Jakaya Mrisho Kikwete Fundation (JMKF) haitakuwa ya kisiasa, na kuwa itafanya kazi na Serikali ya Tanzania na nyingine barani Afrika.

Rais Mstaafu Kikwete ametoa kauli hiyo jijini DSM wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo ya maendeleo JMKF ambapo amesema hakusudii kuwa Mwenyekiti wa Taasisi hiyo maisha.

Kazi kubwa za taasisi hii itakuwa ni kusaidia suala zima la maendeleo ya kijamii, afya hasa afya ya mama na mtoto, lishe na vijana hususan  uongozi na  utawala  bora.

Ad